Jiandae kwa usiku wa burudani usiosahaulika katika ZILIPENDWA Edition, tamasha la vichekesho litakalowaleta pamoja wachekeshaji mahiri kwa maonyesho ya moja kwa moja yaliyojaa vicheko, ubunifu na burudani ya hali ya juu. Njoo ushuhudie vipaji vinavyotikisa jukwaa kwa mizaha ya maisha ya kila siku, utamaduni wa Kitanzania na simulizi zitakazokuacha ukicheka muda wote. Hii ni fursa ya kukutana na marafiki, familia na wapenzi wa burudani katika usiku mmoja wa kipekee jijini Geita. Usikose! Karibu uje ucheke, uburudike na utengeneze kumbukumbu nzuri katika 2iipendwa Edition – Live Comedy Show in Geita, ambapo vicheko havina mwisho! 🎤😂